- 1,684 viewsDuration: 3:16Kwa mara nyingine walipa ushuru nchini wanakodolea macho mzigo mwingine mkubwa wa kifedha wa shilingi bilioni 3.2. Haya yanajiri baada ya kufutiliwa mbali kwa kandarasi ya mafuta ya mabilioni ya pesa kabla ya shehena hiyo kufika Bandari ya Mombasa. Kamati ya Seneti ya Kawi sasa inachunguza mazingira ya utoaji na kufutwa kwa kandarasi hiyo, huku hofu ikitanda kuwa Kenya inaweza kuwa miongoni mwa mataifa yatakayoathirika zaidi iwapo mzozo wa Mashariki ya Kati utaendelea