Skip to main content
Skip to main content

Wanafunzi wanazidi kuhangaikia karo

  • | Citizen TV
    159 views
    Duration: 1:30
    Miongoni mwa wanafunzi ambao hawajapata fursa ya kujiunga na shule ya upili kwasababu ya kukosa karo na pesa za mahitaji mengine ni wasichana wawili Mercy Mwende aliyepata alama 59 pamoja na Alice Auma aliyepata alama 47. Wawili hao walioteuliwa kujiunga na shule za bweni walilazimika kutafuta nafasi katika shule ya Upili ya wasichana ya Lavington ambapo pia hawakufanikiwa kupata pesa zilizohitajika ili kugharamia Karo na sare .Wazazi wao wamekuwa wakiandamana kwa wiki tatu sasa na watoto wao wakijaribu kutafuta ufadhili kupitia kwa basari lakini juhudi zao ziliambulia patupu. Wazazi hao wanadai kuwa hawakuruhusiwa shuleni kwa kukosa shilingi 31,800 za kulipia sare .