- 293 viewsDuration: 1:43Baadhi ya wanasiasa wa Kaunti ya Wajir sasa wanaitaka Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC kuangazia upya muda wa usajili wa wapiga kura, wakisema kuwa mpango wa sasa hauzingatii changamoto za wakazi wa maeneo kame. Wanasiasa hao wanasema kwamba Wajir, haiwezi kulinganishwa na maeneo madogo ambayo hupewa muda sawa wa usajili licha ya tofauti kubwa za eneo na mazingira.