- 207 viewsDuration: 1:50Tume ya uchaguzi na mipaka IEBC imeonya wanasiasa dhidi ya kuingilia zoezi linaloendelea la usajili wa wapiga kura kwa kujaribu kushawishi jinsi wanavyofanya shughuli zao. Akiongoza mkutano wa uhamasisho mjini Hola kaunti ya Tana River,naibu mwenyekiti wa tume hiyo Fahima Araphat amehimiza wenyeji wa eneo hilo kutumia fursa uliyosalia kujiandikisha kama wapiga kura ili kupata nafasi ya kufanya maamuzi ya busara wakati wa uchaguzi mkuu ujao.