Skip to main content
Skip to main content

Wandayi amesisitiza kuwa kuna mafuta ya kutosha nchini

  • | Citizen TV
    70 views
    Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi amesema uhaba wa mafuta nchini unaendelea kutatuliwa, akisema upungufu ulioshuhudiwa kwa siku mbili ulisababishwa na changamoto za usimamizi. Wandayi aliyezungumza bungeni leo, aliwataka wakenya kuwa na subira hali hiyo ikiendelea kutatuliwa. Wandayi ametoa hakikisho kuwa licha ya msukosuko katika mataifa ya mashariki ya kati, taifa limeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa kuna mafuta ya kutosha nchini.