Skip to main content
Skip to main content

Wasamaria wema wahimizwa kujitokeza kutoa msaada kwa wanafunzi waliokwama nyumbani

  • | Citizen TV
    233 views
    Duration: 1:22
    Wadau wa elimu huko Kapsabet wamewahimiza wafadhili na wasamaria wema kujitokeza kuwasaidia wanafunzi wasiojiweza na ambao bado wako nyumbani kwa kukosa karo ya shule. Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa ufadhili wa masomo wa Elimu Scholarship mjini Kapsabet, wadau hao wamesema changamoto ya karo inaendelea kuwanyima maelfu ya watoto fursa ya kuendelea na masomo yao.Mkurugenzi wa Wakfu wa Jomo Kenyatta, Stellah Ruto, amesisitiza umuhimu wa mashirika mbalimbali, sekta binafsi na watu binafsi kushirikiana ili kuhakikisha hakuna mtoto anayekosa elimu kwa sababu ya umaskini.