Washikadau wa elimu wataka elimu ya uzazi ifunzwe shuleni

  • | Citizen TV
    92 views

    Washikadau katika sekta ya afya ya uzazi wameshinikiza kujumuishwa kwa elimu ya afya ya uzazi kwenye mitaala ili kukabili mimba za utotoni na maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Wakizungumza kwenye kongomano la haki za afya ya uzazi kwa vijana huko Kwale, wadau hao wamesema watoto na vijana wa umri mdogo wanaendelea kupata ujauzito na kuambikizwa maradhi ya zinaa licha ya juhudi zinazowekwa kukomesha visa hivyo.