Wasiwasi umezidi kuhusu ongezeko la visa vya ndoa za utotoni katika eneo la Baringo Kusini.
Kwenye kongamano lililowaleta pamoja wakuu wa shule, wenyekiti wa bodi za shule na wasimamizi wa serikali za mitaa, ilibainika kuwa mimba za uttoni zimeathiri vibaya masomo ya wasichana eneo hilo. Washiriki walieleza hofu kuwa licha ya juhudi zinazoendelea za kuhakikisha watoto wanasalia shuleni, baadhi ya wanajamii bado wanaendeleza mila na desturi zinazotatiza elimu. Walimu na wasimamizi wa shule walitakiwa kuwajibika kwa kuripoti matukio hayo mara moja na kuwalinda wanafunzi walio chini ya uangalizi wao.