Watu wanne wajeruhiwa kwenye uvamizi katika kaunti ya Samburu

  • | Citizen TV
    148 views

    Afisa wa zamani wa kijeshi ni miongoni mwa majeruhi wanne wa uvamizi wa punde wa wizi wa mifugo uliotokea katika eneo la Lolmolog Samburu Magharibi. Majangili wa wizi wa Mifugo wanaaminika kufanikisha jaribio la wizi wa mifugo na kuwajeruhi wanne hao kabla vikosi vya usalama kuwathibiti.