- 1,194 viewsDuration: 3:15Watu wawili wamefariki baada ya kupigwa risasi kwenye maandamano yaliyofanyika huko Ishiara, eneobunge la Mbeere North, kaunti ya Embu. Inaarifiwa kuwa maafisa wa polisi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakipinga hali duni ya huduma za afya zinazotolewa katika Hospitali ya Ishiara Level Four. Wakazi wanalalamikia ukosefu wa dawa na vifaa pamoja na miundombinu duni. Hospitali kadhaa nchini zinadaiwa kuwa katika hali sawia, jambo ambalo linasababisha maafa ambayo yangeweza kuepukika.