Skip to main content
Skip to main content

Waumini wa kanisa la Akorino watofautiana kuhusu mwaliko wao Ikuluni jana

  • | Citizen TV
    12,987 views
    Duration: 2:01
    Kundi la waumini wa dini ya Akorino Lililokosa kufika ikulu Jumapili, limeonya dhidi ya Imani hiyo kutumika kufikia malengo ya kisiasa, baada ya baadhi yao kutemwa kwenye mwaliko wa kuabudu ikuluni. Waumini hao, waliofanya ibada mbadala ugani General Matenjagwo eneo bunge la Kandara na kumteua Msemaji wao mpya, wamemuonya Rais William Ruto dhidi ya kuigawanya Imani hiyo, kwa manufaa ya kujifaidi Mwenyewe. Akiahidi kuwaongoza kwa misingi dhabiti inayoongoza Imani hio baada ya kutunukiwa wadhifa huo, simon Mwaura ambaye pia ni Mwakilishi wadi wa eneo la ng’araria na askofu wa kanisa hilo, amewataka waliofika ikuluni kutotumika kuligawanya dhehebu hilo, ambalo limesheni umoja na amani kwa miaka mingi.