- 319 viewsDuration: 2:24Waziri wa afya Aden Duale ametoa wito kwa wamiliki wa hospitali za kibinafsi nchini kutumia mbinu rasmi katika kujadiliana na wizara yake ili kutoa nafasi ya kutatuliwa kwa matatizo hasa ya malipo yanayotokana na bima ya kitaifa ya (SHA).Akizungumza katika kikao kilichowaleta pamoja wamiliki wa vituo vya afya vya kibinafsi na maafisa wa ngazi za juu katika wizara ya afya, Duale alikosoa muungano wa hospitali za kibinafsi (RUPHA) kwa kujadili matatizo yanayozonga sekta hiyo kupitia vyombo vya habari kabla ya kutafuta suluhu kupitia njia rasmi.