Zaidi ya mitungi ya gesi 19 ya uvuvi yanaswa Lamu

  • | Citizen TV
    1,232 views

    Zaidi ya mitungi ya gesi 19 ya uvuvi haramu imenaswa na wavuvi wa Lamu katika eneo la Manda Bruno bahari ya Lamu. Kwa miaka mingi sasa, Wavuvi Lamu wamekuwa wakilalamikia kukithiri kwa visa vya uvuvi haramu unaotekelezwa na wavuvi kutoka nje ya kaunti ya Lamu. Ni uvuvi ambao umelaumiwa kwa kusababisha kupungua kwa viwango vya samaki baharini.