Zaidi ya watu milioni 1.4 kutoka kaunti sita za Nyanza bado hawajajisajili kama wapga kura, licha ya kuwa na vitambulisho. Akitoa takwimu hizo, mratibu katika eneo la Nyanza Flora Mworoa alisema kuwa afisi yake inashirikiana na asasi mbali mbali wakiwemo machifu kuhakikisha kuwa usajili unaimarishwa, katika siku tano zilizosalia. Mworoa pia alisema kuwa zaidi ya vitambulisho elfu themanini havijachukuliwa, hali hiyo ikiathiri mipango maalum ya serikali. Jumanne wiki ijayo IEBC itakamilisha shuguli ya usajili maalum ya halaiki, na usajili huo kurejea katika afisi za maeneo bunge.