
80,247 views
Hivi wewe unaiunga mkono?
Tazama mke wa kwanza akimkaribisha mke wa pili madhabahuni! 😮 Mchungaji mmoja nchini Marekani amezua gumzo mtandaoni baada ya kumtambulisha hadharani mke wake wa pili kanisani, huku mke wake wa kwanza akimuunga mkono mbele ya waumini. Israel T. Ford, mwanzilishi wa kanisa la LifeWorks Church katika jimbo la Ohio, alimkaribisha Shakayla Ford wakati wa ibada. Kilichowashangaza wengi ni jinsi mke wake wa kwanza, Lydia Ford, ambaye pia ni mchungaji mwenza, alivyompokea Shakayla na kumtaja kama "dada yangu katika ndoa" “. Je, unaunga mkono ndoa ya mke zaidi ya mmoja katika Ukristo? Kwa nini? Tuambie maoni yako kwenye sehemu ya maoni! Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw
- Walimu 5 hatiani kwa kuwanyanyasa wanafunzi wa kiume kingono
- Wushu: Sanaa ya mapigano inayovutia vijana wa Kenya.
- ‘Tutakuwa na katiba mpya 2029’ asema Samia Suluhu Hassan. Katika Dira ya Dunia TV
- Matangazo ya Dira ya Dunia Redio 20/ 11 /2026
- Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aahidi kuwepo kwa katiba mpya ifikapo mwaka 2029.
- Soka Tanzania: Simba kutawala au Yanga kurudi kwa kishindo?
- Mbunge ageuza hotuba ya kuaga bungeni kuwa pendekezo la ndoa
- AMKA NA BBC - NOVEMBER 20' 2026