Skip to main content
Skip to main content

Wadau wa elimu Nairobi waiomba serikali kuzingatia elimu ya ujuzi na vitendo katika mtaala mpya

  • | Citizen TV
    141 views
    Duration: 3:54
    Baadhi ya wadau wa elimu hapa Nairobi wanaiarifu serikali kuzingatia zaidi elimu ya mafunzo ya ujuzi kwa wanafunzi (skill-based education) ili kizazi cha sasa na kijacho kinuafike zaidi na mfumo wa sasa wa elimu. Wakiongozwa na Jacob Mututi, ambaye ni mkuu wa shule ya Kinderworld Academy, wadau hao pia wameitaka serikali kuongeza juhudi katika masomo ya vitendo kwenye mtaala mpya wa elimu ili kuchochea vipaji miongoni mwa wanafunzi. Aidha, wameipongeza serikali kwa jinsi ilivyosaidia kusawazisha matokeo ya mtihani wa kitaifa wa KJSEA mwaka huu, wakisema hakukuwa na tashwishi licha ya kuwa ni mfumo wa kipekee ukilinganisha na ule wa 8-4-4.