- 494 viewsDuration: 1:41Kijana mmoja wa miaka 30 amepatikana ameuawa na genge la watu wasiojulikana Kwa kudungwa na visu. Martin Wangoto ambaye alikuwa fundi wa magari Jijini Nakuru alidungwa kisu tumboni mwendo wa saa sita usiku Katika eneo la Rhonda, Nakuru Magharibi. Haya yanajiri huku visa vya utovu wa usalama vikizidi kuripotiwa Katika eneo hilo. Sasa wakazi wanawataka maafisa wa polisi kuwajibika zaidi. Mwili wa muathiriwa ulipelekwa Katika makafani ya rufaa ya Nakuru Annex.