- 1,278 viewsDuration: 1:24Chama cha UDA kimesistiza kwamba taratibu ya kutekeleza agenda kumi walizokubaliana na ODM Mwaka jana zingalipo na kwamba Mazungumzo mapya na ODM hayataathiri mipango ya awali. Wakizungumza katika makao makuu ya chama, viongozi wa UDA walisema kuwa mazungumzo hayo yanalenga kujenga uhusiano wa muda mrefu hata baada ya uchaguzi wa mwaka 2027. Pia waliwahakikishia wafuasi kuwa majadiliano na ODM hayataathiri uhusiano wa UDA na vyama vingine kwenye Muungano wa Kenya Kwanza