Skip to main content
Skip to main content

Wanafunzi wengi wanendelea kuhangaika nyumbani

  • | Citizen TV
    291 views
    Duration: 3:20
    Nje ya afisi ya chifu wa Mtwapa kaunti ya Kilifi wanafunzi wa gredi ya 10 walifurika nje na ndani wakisaka nafasi za shule za kutwa zilizoko katika kata hii. Wakiandamana na wazazi wao wanasema ukosefu wa karo umewalazimu kubadili nia na kujiunga na shule za kutwa ili wanawe wapate masomo. David ramadhan mwanafunzi wa shule ya shimo la tewa alipata alama 57 na kuitwa shule ya st george's kaloleni nafasi hiyo huenda ikamponyoka kutokana na ukosefu wa karo. Ups david ramadhan mwanafunzi ups mohammed raka mzazi muda wa kujiunga na shule ukiwa umekamilika hofu kwa wanafunzi na wazazi ni kuendelea kukosa masomo kwa wanafunzi hawa zaidi ya 100 katika kata hii huku wazazi wakidai kuwa wanafunzi zaidi bado wapo nyumbani.