Waziri Aisha Jumwa awatetea wabunge 'waasi' wa ODM

  • | K24 Video
    31 views

    Viongozi wa Kenya Kwanza waliohudhuria hafla ya kutoa shukrani katika kanisa la ACK Gede kaunti ya Kilifi wamekikemea chama cha ODM kwa kuwafurusha kutoka chamani baadhi ya wabunge kwa madai ya kushirikiana na serikali ya Kenya Kwanza. Wakiongozwa na mkuu wa wafanyikazi wa umma Felix Kosgei pamoja na waziri wa utumishi wa umma na jinsia Aisha Jumwa wamekikashifu chama cha ODM kwa kutoonyesha usawa kuhusiana na kanuni zake dhidi ya wanachama waasi.