Seikali za kaunti kuongeza ushuru kuziba pengo la ushuru

  • | K24 Video
    30 views

    Baadhi ya magavana sasa wanatishia kuwatoza wakenya ushuru sawia na unaotozwa na serikali kuu kufuatia vuta ni kuvute ya ugavi wa rasilimali iliopelekea mkutano wa leo baina ya serikali ya kitaifa na za kaunti kutibuka bila maafikiano. Baraza la magavana linashikilia ni sharti wapokee shilingi bilioni mia nne hamsini katika mwaka wa kifedha ujao ingawa tume ya ugavi wa rasilimali CRA inapendekeza shilingi bilioni mia tatu tisini na nane ilhali wizara ya fedha inasema ina uwezo wa kutoa shilingi bilioni mia tatu tisini na moja tu