Afueni kwa watoto wa kurandaranda kaunti ya Busia baada ya kufunguliwa kwa shule ya msingi

  • | Citizen TV
    143 views

    Ni afueni kwa watoto wa kurandaranda mitaani na wale kutoka familia zisizojiweza katika kaunti ya Busia baada ya kufunguliwa kwa shule ya msingi ambayo inakusudiwa kuwapa elimu bure. Idadi ya watoto wa kurandaranda mitaani na familia zao imeongezeka pakubwa katika kaunti ya Busia huku wengi wao wakitoka nchi jirani ya Uganda na kupiga kambi kwenye mitaa ya Busia na Malaba.