Jamaa na marafiki wajumuika na mzee Peter Kivuva baada ya kufikisha miaka 102

  • | Citizen TV
    2,144 views

    Huku Waksristo wakikamilisha sikukuu za pasaka hii leo familia moja kaunti ya Machakos ilisherekea sikukuu hiyo kwa njia ya kipekee baada ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mzee wao aliyefikisha miaka 102. Mzee Peter Kivuva alimiminiwa sifa kutokana na hali yake ya afya hadi sasa, kwani bado anajitegemea kwa kazi za kawaida za nyumbani. Kwa upande wake, Kivuva alisema kuwa hali yake ya afya imechangiwa na kula vyakula vya kiasili na kufanya mazoezi mara kwa mara