9,454 views
Duration: 4:28
Mrengo wa upinzani umepuuzilia mbali tetesi za kusambaratika. Katika hali ya kudhihiri umoja, viongozi wote wa upinzani walihudhuria kongamano la kitaifa la wajumbe la chama cha Wiper, ambapo Kalonzo Musyoka aliidhinishwa kuwa mwaniaji rasmi wa kiti cha urais kwa chama hicho. Mkutano huo ulionekana kama mkakati wa chama hicho wa kuunganisha mrengo wa upinzani tayari kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 na vilevile azimio la upinzani la kumuunga mkono Kalonzo Musyoka iwapo uteuzi wa mwaniaji wa muungano wa upinzani utampendelea.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive