
468,141 views
6 Dec 2024
Lyrics *Tabibu Mkuu Yesu aletaye faraja kwetu, Mwenye huruma nyingi, Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.* 1. *Pindi tuwapo wagonjwa, twatafuta madakitari, washindwapo twaugua nini, ndipo waita wataalamu. Yaweza chukua muda mrefu, huenda hata miaka, kupata utambuzi sahihi, miili yetu iuguayo.* 2. *Hata hivyo tunaye, tabibu mmoja wa kweli, hahitaji miadi kumwona, anahudumu wakati wote. Hakuna bima, madawa, matibabu yake ni bure, majibu ya yale uuguayo yeye Mungu anajua.* 3. *Tenga muda rafiki naye muuguzi wa ajabu, upate ukaguzi maalum, kuelewa ikuumizayo. Mweleze unavyohisi, kimwili, hisia, kiroho. Usimtafute tu Mungu wakati afya yako idororapo.*
