
378,168 views
24 Nov 2023
Video Prodcued By : Enovarts Creatives Director : LeyMan DoP : Frickern Ass. Director : Osteen, Webster Gaffer & Lighting : Steve Inyangala & Emma Alex Makeup Artist : Oasis Beauty Spa Styling : Diana Dee LYRICS *MUNGU MTUNZA AGANO* *1.Mungu wetu mtunza agano mtimiza ahadi alotoa, ajibuye maombi ya Imani, tumai la wakosa tumaini. Mpiga vita vyema usiyeshindwa, mtenda miujiza kwetu sisi, mtengeza njia baharini, maji safi atunywesha jangwani* *Mungu wa hekima tangu mwanzo, Jehova Jireh Mpaji wa vyote, El-shadai Mungu Mwenyezi, Adonai ndiye Bwana wetu. Alfa Omega mwanzo na mwisho, Ebeneza hadi umbali huu...Immanueli Mungu yu nasi, Elohim Mungu muumbaji* *2.Mshauri wa ajabu kwa mambo yote, Mungu mwenye nguvu mpisheni, Baba wa milele aishiye, Mfalme wa amani kwa mataifa, Tabibu mkuu asiyelala, Mume wa wajane asiyetaliki, Baba wa mayatima mwenye huruma, Mungu wa upendo apewe sifa* *3.Muumbaji wa vyote Mbingu na Dunia , Tasa wananyonyesha kwa jina lako Msogeza milima ni Mungu pekee, Mwanga kwenye Giza haufichiki, Mungu mwenye nguvu hulinganishwi, Mfadhili wa wahitaji hubadiliki, watuepusha majaribu hautikisiki, Mungu uu mmoja haufananishwi*
