
347,243 views
24 Dec 2020
LYRICS Jihoji moyoni mwako ukishapimwa kwenye miizani, mazuri yamezidi mbaya u moto baridi, Mimi sijafika kwa Imani nasonga mbele makao yaningoja alipo Bwana niwe naye. 1. Mungu ameuhesabu ufalme wako tena ameukomesha kwani umepimwa, Mizani ya Bwana yaonyesha umepunguka na ufalme wako umegawanyika, Usiku huo Belishaza wa kalidayo kauwawa Dario ka pokea Ufalme, Mungu ni mwaminifu, neno lake thabiti, anayejikweza hakika atashushwa. 2. Mbona mwabudu fedha Miungu yenu dhahabu ya shaba na ya chuma, miti hata ya mawe yote kazi ya mikono ya wanadamu, Zina vinywa havisemi macho ambayo hayaoni masikio hayasikii mapua hayanusi, mikono yao haishiki wala miguu haiendi walimwrngu siabudu sanamu Mungu wetu Yu hai. 3. Timazi imeteremshwa kutani mwako mpendwa je umepinda umelainika Jiulize je, hadhi yako inatatanisha simama uwe shuhuda, Mungu ni yule yule wa jana, leo hata Milele.
