
671 views
27 Nov 2026
LYRICS Chorus *Waweza elewa tu wimbo wa ushindi kama ulikuwa vitani.* 1. *Umewahi ugua mwenyeji hospitali, neema ikashuka ukapata afueni. Je umehangaishwa na maadui wako usisahau Mungu yupo wimbo wa ushindi utaimba.* 2. *Wakati wa hitaji msamaria mwema alipitia kwako sasa waelewa wimbo huu Bwana akaugeuza kilio kuwa kicheko, mazito yakawa mepesi sasa waimba wimbo huu.* 3. *Umekuwa vitani na mapepo ya giza. Umeomba sana bila mafanikio. Usife moyo mpendwa, Mungu yupo kazini anafanya mambo yake mwishowe utaimba wimbo huu.* *Bridge* *Kila kovu lina hadithi kila machozi ushuhuda huu si wimbo wa kawaida ni wimbo wa walioshinda.*
