Skip to main content
Skip to main content

Hofu ya visa vya utekaji nyara wa watoto yaongezeka baada ya mtoto kuokolewa Githurai

  • | Citizen TV
    18,656 views
    Duration: 4:01
    Jioni ya leo, tunaanza taarifa zetu kwa hofu ya kuongezeka kwa visa vya utekaji wa watoto katika maeneo mbalimbali nchini. Kisa cha hivi punde ni kuokolewa kwa mtoto wa miaka miwili aliyedaiwa kutekwa katika mtaa wa Kiuu, Githurai jijini Nairobi. Kamera za CCTV zilinasa tukio hilo, huku msichana mwenye umri wa miaka 15 akidaiwa kuwaambia wachunguzi kuwa alitumwa kumchukua mtoto huyo kwa ahadi ya kupewa zawadi. Kizaazaa kilishuhudiwa wakati wa operesheni ya kumuokoa mtoto huyo, huku wapelelezi wakiamini kuwa huenda visa vya aina hiyo vina uhusiano na shughuli zinazochunguzwa katika eneo alikopatikana mtoto huyo.