- 112 viewsDuration: 1:34Jamii ya Ogiek inayoishi katika eneo la Chepkitale, Mlima Elgon, imeathirika baada ya barabara pekee inayounganisha eneo hilo na Kapsokwony kuharibiwa na mafuriko. Wakazi hao wanasema barabara hiyo ya kilomita 34 iko katika hali mbaya, jambo linalohatarisha maisha yao na kuwazuia kupata huduma muhimu. Aidha, wakazi wamelalamika kuwa bidhaa zao za kiuchumi kama maziwa na asali haziwezi kufikishwa sokoni kutokana na hali duni ya barabara hiyo iliyopuuzwa kwa miaka mingi.