- 1,234 viewsDuration: 1:22Mabweni matatu ya shule ya wavulana ya Matungulu kaunti ndogo ya Kangundo yameteketea kufuatia mkasa wa moto uliotokea mapema hii leo. Moto huo uliosababisha kujeruhiwa kwa wanafunzi 15 uliteketeza vitanda na magodoro pamoja na vifaa vya shule. Chanzo cha moto huo hakijabainika huku shule ikisema inatafakari mustakabali wa shule hiyo kwani sehemu kubwa inayotumika na wanafunzi imeteketea.