- 252 viewsDuration: 1:35Muungano wa Walimu wa KUPPET na Mamlaka ya Afya SHA wamefikia makubaliano ya kuondoa malipo ya matibabu kwa walimu, hatua itakayowawezesha kupokea huduma za afya bila kuwekwa viwango vya juu au kulazimika kulipa kutoka mifukoni mwao. KUPPET pia imewahakikishia wazazi na wanafunzi kuwa shule zitafunguliwa kama ilivyopangwa, huku ikipuuza tishio la mgomo lililotolewa na baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaopinga kile wanachodai ni huduma duni za afya chini ya SHA.