Skip to main content
Skip to main content

Mama afariki Nyeri baada ya kujifungua kwa upasuaji

  • | Citizen TV
    9,073 views
    Duration: 3:16
    Familia moja huko kambura-ini eneo bunge la kieni kaunti ya Nyeri, inaitaka hospitali ya Naromoru level 4 kuchukuliwa hatua, baada ya binti yao Joy Kiende mwenye umri wa miaka 19 kufariki wakati wa kujifungua kwa njia ya upasuaji. Kulingana na mumewe James Munene, Joy alikuwa buheri wa afya kufikia Ijumaa ya tarehe 27 mwezi jana kabla ya upasuaji huo kufanyika, ila akaaga siku tano baadaye akipokea matibabu zaidi kwenye hospitali ya rufaa ya Nyeri.