Skip to main content
Skip to main content

Maraga akemea ugawaji wa maeneo ya kisiasa, ataka uchaguzi huru nchini

  • | Citizen TV
    372 views
    Duration: 1:17
    Kinara chama cha UGM David Maraga amekashifu njama ya vyama vya kisiasa kutenga maeneo ambayo yatatengewa vyama vyenye ushawishi mkubwa katika maeneo hayo. Maraga anasema kuwa mkondo huo utazidi kuwagawanya wakenya na zaidi kuwanyima uhuru na haki ya kuwachagua viongozi wanaofaa. Akizungumza wakati wa ziara yake kaunti ya Siaya, jaji huyo mkuu wa zamani amesema swala hilo linatishia kudhoofisha demokrasia. Aidha Maraga amezidi kukashifu hulka ya kutumia wahuni kuvuruga mikutano ya upinzani.