- 991 viewsWanafunzi wanne zaidi walioangamia kwenye mkasa wa moto katika shule ya wasichana ya Utumishi wamezikwa leo, kwenye hafla za mazishi zilizojaa huzuni na majonzi tele. Familia, jamaa na marafiki wakijumuika maeneo tofauti kuwaaga wanafunzi hawa waliokuwa kati ya wanafunzi 16 walioteketea kwenye mkasa huo. Mwanafunzi mmoja Neema Wairimu atapumzishwa siku ya Jumatano eneo la Ruai hapa Nairobi