Skip to main content
Skip to main content

Mkaguzi Mkuu afichua upungufu wa KSh 903m katika ufadhili wa shule za umma

  • | Citizen TV
    310 views
    Duration: 3:43
    Zaidi ya shilingi milioni 903 zilizotengwa na hazina ya kitaifa ya fedha kufadhili masomo ya wanafunzi katika shule za umma kati ya mwaka wa 2020 - 2024 hazikutumwa shuleni. Kulingana na ripoti maalum ya mkaguzi wa hesabu za serikali, fedha hizo zilikuwa sehemu ya shilingi bilioni 334.1 zilizotengewa shule za sekondari, sekondari msingi na shule za msingi za umma kufanikisha masomo. Haya yakijiri licha ya lalama za walimu kuwa fedha hizo zinazotolewa hazitoshi na zinachelewa sana. Na kama anavyoarifu serfine achieng ouma, walimu wakuu wanasema hawajapokea fedha zilizoahidiwa kutumwa kabla ya muhula wa pili kuanza.