Msajili wa mahakama Anne Amadi apata afueni

  • | Citizen TV
    287 views

    Ni afueni kwa Msajili wa Mahakama Anne Amadi baada ya mahakama kutupilia mbali agizo la kufungwa kwa akaunti zake. Hii inamanisha kuwa amadi sasa ataweza kutumia akaunti zake ambazo zilikuwa zimefungw amwezi uliopita kufuatia kesi ya dhahabu ghushi. Jaji Alfred Mabeya amesema kuwa hakukuwa na ushahidikuwa amadi alihusika na shughuli zilizokuwa zikiendeshwa na kampuni ya uwakili ya Amadi and Amadi Associates au kuwa alifaidi pesa hizo. Kampuni moja ya Dubai imemtaja Amadi na mwanawe Brian Ochieng kwenye kesi ambapo kampuni hiyo inadai kulipa shilingi milioni 89 kununua kilo 1,500 za dhahabu ila haikupata dhahabu hiyo.