Mshukiwa mmoja kati ya 3 wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya Albert Ojwang

  • | Citizen TV
    11,282 views

    Haya yalipokuwa yakijiri, halmshauri ya utendakazi wa polisi IPOA imeripoti kuwa maafisa wa usalama wanamzuilia mshukiwa mmoja kati ya watatu waliohusishwa na mauaji ya Albert Ojwang. Mwenyekiti wa IPOA Isaack Hassan ameiambia kamati ya usalama katika bunge la kitaifa kuwa, kanda ya CCTV ilifutwa kimakusudi kutatiza uchunguzi wa mauaji ya Ojwang. Aidha, Inspekta Mkuu wa polisi Douglas Kanja naye akisema naibu wake atalazimika kujiondoa endapo atatajwa kwenye uchunguzi unaoendelea.