- 2,700 viewsDuration: 2:50Viongozi wa Kenya Kwanza wakiongozwa na naibu wa rais Kithure Kindiki wamemkashifu aliyekua naibu wa rais Rigathi Gachagua kwa matamshi yake ya kupinga miradi wa serikali. Viongozi hao wamesema matamshi ya Gachagua kuwa atasitisha baadhi ya miradi ya serikali iwapo atachaguliwa rais yanayumbisha maendeleo katika taifa na kurudisha nyuma maisha ya wananchi. Viongozi hao wanashikilia kuwa miradi inayofanywa sasa inamanufa akwa wakenya na watafanya kila juhudi kuhakikisha Rais William Ruto anachaguliwa kwa muhula wa pili.