- 1,453 viewsDuration: 2:51Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja alisema tayari wamewatuma maafisa wa usalama kwenye barabara kuu nchini kuhakikisha mfumo wa kulipa faini mara moja kwa madereva wanaovunja sheria unaanza msimu huu wa sikukuu. Ni shughuli ambayo tayari imeanza katika baadhi ya barabara kuu nchini ikiwemo ile ya Nairobi - Nakuru.