Skip to main content
Skip to main content

Polisi adaiwa kumpiga risasi na kumjeruhi mkazi Isebania

  • | Citizen TV
    2,923 views
    Duration: 2:32
    Familia Moja katika eneo la Isebania inalilia haki baada ya mwana wao kupigwa risasi na maafisa wa polisi . Kulingana na familia ya James Chacha Marwa, mwenye umri wa 35, alipigwa risasi na afisa wa polisi kwa tuhuma za kuiba gari—tuhuma ambazo baadaye zilibainika kuwa si za kweli.. Marwa alikuwa amekamatwa kwa kushukiwa kuiba gari na baadaye kuachiliwa huru. Familia hiyo sasa inataka polisi aliyehusika akamatwe na kushtakiwa.