Polisi wachunguza ulanguzi wa watoto Mlolongo

  • | Citizen TV
    1,212 views

    Maafisa wa usalama katika eneo la Mlolongo, Kaunti ya Machakos wanamzuilia mwanamke mmoja aliyekiri kuhusika na biashara haramu ya kuwaiba na kuwauza watoto. Miriam Wesonga alikamatwa mapema leo, miezi mitatu baada ya kuhusishwa na wizi wa mtoto wa miaka miwili unusu. Mtoto huyo alipatikana eneo la Matungu kaunti ya Kakamega, akikubali kushirikiana na wenzake kwenye biashara hiyo.