Rais William Ruto amemtetea mwenyekiti wa chama cha KANU Gideon Moi kuhusu uamuzi wake wa kujiondoa kutoka uwaniaji wa kiti cha Useneta kaunti ya Baringo, na kukubali kufanya kazi na serikali yake. Akizungumza huko Kabarak ambako Gideon alikuwa mwenyeji wa wafuasi wa chama cha KANU, Rais alisema seneta huyo wa zamani wa Baringo hakukosea kuisaidia serikali yake kuimarisha umoja wa kisiasa na kubadilisha taifa. Rais sasa ametaka makubaliano rasmi na chama cha KANU kujiunga na serikali jumuishi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive