Serikali yajenga shule tano maalum mpakani wa kaunti za Elgeyo Marakwet, Baringo na Pokot

  • | Citizen TV
    241 views

    Waziri wa Usalama Professor Kithure Kindiki amesema kuwa serikali itajenga shule tano maalum chini ya mpango wa amani. Shule hizo za kijamii za Dira, Todo, Tuwit, Lomuke, na Chepchoren zitahakikisha wanafunzi kutoka kaunti za Elgeyo Marakwet, Baringo na Pokot Magharibi wanapata mafunzo ili waweze kubadili vizazi vijavyo, na kueneza amani na utangamano katika kaunti hizo ambazo zinashughudia mapigano ya mara kwa mara kutokana na wizi wa mifugo. Waziri wa usalama amesema utangamano wa wanafunzi kutoka jamii hizo utapunguza uhalifu na uhasama wa kijamii.