Serikali yapunguza ushuru wa mchele kutoka nje ushuru wa bidhaa ya anasa kama vileo kuongezeka

  • | Citizen TV
    3,222 views

    Ni afueni kwa wanaofanya biashara ya mchele baada ya serikali kupunguza ushuru wa kuagiza bidhaa hii kutoka mataifa ya nje. Aidha, wajenzi na wanaofanya kazi ya bidhaa za ngozi pia wamepata afueni kwenye bajeti ya mwaka huu. Akisoma bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2025/26, waziri wa hazina kuu ya kitaifa John Mbadi ametangaza kuongezwa kwa ushuru wa bidhaa ya vileo, huku wageni wanaofanya biashara za pesa za kimtandao sasa wakitakiwa kulipa ushuru wa VAT.