Shirika la FAO laonya uvamizi wa viwavi katika kaunti 23

  • | Citizen TV
    192 views

    Shirika la chakula duniani - FAO - limetoa tahadhari ya kusambaa kwa viwavi jeshi katika zaidi ya kaunti 20 huku nchi sita Afrika Mashariki zikiathirika. Shirika la FAO linasema kuwa msambao huo umesababishwa na mabadiliko ya tabianchi. FAO inasema hali hii inahatarisha utoshelevu wa chakula kwani maeneo mengo bado yanaathirika na ukame na uvamizi wa nzige. Shirika hilo limetenga dola 500,000 za Marekani kutoa mafunzo kwa maafisa wa nyanjani na kununua vifaa vya kupambana na viwavi jeshi. Mataifa ya Kenya, Eretria, South Sudan, Ethiopia, Somalia na Uganda zimeathirika zaidi.