Siku ya bahari ya kimataifa yaadhimishwa leo kote duniani

  • | Citizen TV
    165 views

    Huku siku ya kimataifa kuhusu bahari ikiadhimishwa hii leo, wataalam katika sekta hio wametaja uchafuzi wa mazingira ya bahari kama tishio kuu kwa viumbe baharini. Wataalmu kutoka shirika la utafiti wa maswala ya bahari KEMFRI wanasema kwamba uchafu mwingi na hasa plastiki ungali unatupwa baharini licha ya serikali kupiga marufuku matumizi ya plastiki. Wataalamu hao wanatoa wito kwa vitengo husika serikslini kuhakikisha kwamba wavuvi wanatumia vifaa vinavyostahili ilikukabiliana na uvuaji wa samaki wadogo.