Takriban visa 800 vya mimba za utotoni viliripotiwa Lamu, 2024

  • | Citizen TV
    323 views

    Visa vya mimba za mapema miongoni mwa wasichana wadogo vimeendelea kuongezeka katika maeneo mbalimbali ya kaunti ya Lamu huku mwaka wa 2024 pekee Lamu iliripoti takriban visa 800 vya wasichana wadogo kupachikwa mimba. Hii ni kwa mujibu wa takwimu kutoka kwa Wizara ya Afya kaunti hiyo.