- 7,557 viewsDuration: 2:56Umoja wa Upinzani umeonya kuwa utamshtaki rasmi Rais William Ruto katika mahakama ya ICC kwa madai ya kutumia magenge ya vijana kutekeleza mashambulizi dhidi ya wanasiasa wa upinzani na pia wizi wa mali. Viongozi hao wakiwemo Kinara wa DCP Rigathi Gachagua na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka waliotamatisha ziara yao Ukambani pia walikosoa serikali kwa kusababisha gharama ya maisha kupanda kupitia kuongezwa kwa bei ya bidhaa muhimu.