- 236 viewsDuration: 1:35Wabunge wa kitaifa kutoka kaunti ya Taita Taveta wamesema watafanya kazi kwa karibu na rais William Ruto kwa minajili ya maendeleo ya wananchi wa kaunti hiyo. Wakizungumza wakati wa hafla ya kupeana basi la shule ya upili ya Ngami huko Mwatate lililotolewa na rais, wabunge hao Peter Shake na Lidya Haika wanasema kamwe viongozi wa kaunti hiyo hawatakubali siasa za upinzani. Vilevile wamesema wataunga mkono utekelezaji wa miradi ya elimu hasa ujenzi wa mabweni katika vyuo vya kiufundi ambao unatekelezwa na serikali kuu.